Uplift Microfinance LtdUplift Microfinance LtdUplift Microfinance Ltd
(Jumatatu - Jumamosi)
info@upliftmicrofinance.co.tz
S.L.P 35059, Dar es Salaam, Tanzania
Uplift Microfinance LtdUplift Microfinance LtdUplift Microfinance Ltd

Kuwawezesha Wajasiriamali Wanawake Kupitia Mkopo wa vikundi

Uplift Microfinance inawawezesha wanawake wa Kitanzania kupitia mkopo wa vikundi unaochochea ushirikiano, uwajibikaji, na uhuru wa kiuchumi

Katika eneo moja pembezoni wa jiji la Dodoma, kikundi cha wanawake wa ushonaji kiitwacho Nguvu Moja kilipokea mkopo wa vikundi wa kiasi cha Tsh milioni 3 kutoka Uplift Microfinance. Fedha hizi ziliwawezesha kununua mashine za ushonaji na kupanua wigo wa wateja wao hadi mashuleni na kwenye taasisi jirani.

“ Kabla ya mkopo huu tulikua tukishona nyumbani. Sasa tuna duka, sare za kusambaza na matumaini kwa watoto wetu”, alisema mwenyekiti wa kikundi Mwanahamsi Juma.

💡 Tunajenga Ustahimilivu pamoja

Mkopo wa vikundi kutoka uplift umelenga kukuza maendeleo ya pamoja na uwajibikaji wa pamoja, kila mshiriki anahakikisha mkopo wa mwenzake hivyo kuunda mfumo imara wa kusaidiana.

“Kila mmoja alikua na ndoto yake. Kwa pamoja tumejenga Biashara.”
Kikundi cha wanawake Nguvu Moja 

Leo hii kikundi hiki kimeajiri wanawake 8 na kinahudumia wateja katika wilaya mbili.